Kolombia

Mwenyeji wa Siku ya Mazingira Duniani mwaka wa 2020

Mambo Muhimu

Watu

Kolombia ni taifa lililo na watu wa makabila mbalimbali. Idadi ya watu nchini humo ni milioni 48. Jamii za watu wa kiasili huishi nchini humo kama ilivyo na mataifa mengine yanayopatikana Amerika ya Latini hasa wakati wavamizi kutoka Uhispania walipowasili huko katika karne ya 15. Aina tatu ya jamii-watu wa kiasili, watu kutoka ulaya na Waafrika-ndiyo watu wanaofanya Kolombia kujivunia utamaduni anuai.

National flag of Colombia

Jiografia

Nchi inayokalia eneo la kilomita milioni 2 mraba, Kolombia ni nchi inayochukuwa nafasi ya nne kwa ukubwa katika eneo la Amerika Kusini na taifa la pekee lililo na pwani katika Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Karibean. Milima inayovutia ya Andea ni milima mipana mno duniani inayoanzia kaskazini hadi kusini mwa nchi. Vilele virefu zaidi vya milima hii vina urefu wa mita 5,775. Eneo la kusini lina misitu ya Amazon, misitu ambao imenea hadi kwa nchi nyinginezo saba.

Historia

Utamaduni wa kiasili ulivuma nchini Kolombia katika karne ya 15. Ilitawaliwa na wakoloni kutoka nchi ya Uhispania kuanzia karne ya 16 hadi mwaka wa 1810. Kipindi hicho kiliitimishwa wakati raia na wasomi walipotia sahihi Sheria za kuleta Mapinduzi, zilizopelekea vita vya kupigania uhuru vilivyohitimishwa Kolombia ilipopata uhuru katika mwaka wa 1819.

Uchumi

Kolombia ni mojawapo wa nchi zilizo na uchumi ulioimarika mno katika eneo la Amerika ya Latini. Nchi hiyo inashikilia nambari ya pili kwa nchi zinazouza maua nje ya nchi na nambari tatu duniani kwa uzalishaji wa kahawa. Kolombia ni nchi mwanachama wa Muungano wa Biashara wa Nchi za Pasifiki ikiwa ni pamoja na Chile, Meksiko, Peru na ina shirikiano wa kibiashara na Marekani na nchi nyinginezo kadhaa.

Mazingira

Kolombia ni mojawapo wa nchi zilizo na bayoanuai nyingi duniani. Zaidi ya aina 51,000 ya viumbe hupatikana nchini humo. Ina aina mbalimabali ya ndege na inayozalisha maua duniani na inashikilia nambari mbili duniani kwa kuwa na mimea, vipepeo, samaki wa maji yasiyo na chumvi na amfibia wa aina mbalimbali.

Viumbe hawa wote wananufaika kutokana na kuwepo kwa aina na mifumo ya ekolojia zaidi ya 300. Baadhi ya mifumo hiyo imehifadhiwa vizuri na haijaaribiwa kamwe.