Bayoanuai

Bayoanuai ni nguzo ya maisha duniani na nguzo ya maendeleo yanayofanywa na binadamu.

Siku ya Mazingira Duniani ya mwaka wa 2020 inatoa wito wa dharura wa kutunza bayoanwai.

Bayoanwai hurejelea viumbe mbalimbali wanaopatikana duniani. Inajumuisha aina milioni 8 ya viumbe wanaopatikana duniani–kuanzia kwa mimea na wanyama hadi kwa kuvu na bakteria; mifumo ya ekolojia inayotumika kama makazi; na uanwai wa kimaumbile.

Bayoanuai inaweza kuonekana kama utandu ambao kila sehemu inategemeana. Sehemu moja ikibadilishwa–au ikiondolewa–mfumo mzima unaathiriwa, na matokeo yanaweza kuwa chanya au ghasi.

Huduma kutoka kwa Mazingira

Mazingira hukabiliana na baadhi ya changamoto anazokumbana nazo mwanadamu. Hutupa oksijeni, husafisha maji tunayokunywa, huhakikisha mchanga una rutuba, na hutupa aina mbalimbali ya vyakula tunavyohitaji ili kuwa na afya njema na kukabiliana na magonjwa. Husaidia watafiti wa masuala ya afya kuelewa fiziolojia ya binadamu; na kutupa vifaa vya kutumia kuunda madawa. Yamepelekea kuanzishwa kwa viwanda vingi na kutoa mapato. Pia, husaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuhifadhi kaboni na kuwezesha mvua kunyesha. Maisha hayangewezekana duniani bila huduma kutoka kwa mazingira. Yana manufaa mengi mno

Mahitaji ya Binadamu

Na mahitaji yetu yanayoongezeka, watu wametumia mazingira kuliko yanayoweza kustahimili. Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita, idadi ya watu duniani imeongezeka mara dufu; uchumi wa kimataifa umeimarika karibu mara nne zaidi na biashara ya kimataifa imeongezeka takribani mara kumi zaidi. Itachukua uongezekaji wa dunia na kuwa 1.6 ili kuweza kukidhi mahitaji ya binadamu kila mwaka.

Kuzuka kwa virusi vya COVID-19 ni ishara tosha kuwa tukiharibu bayoanuai, tunaharibu mfumo ambao huwezesha binadamu kuishi. Kwa kuathiri mazingira, tumesababisha uwezo wa vijidudu vinavyosababisha magongwa ikiwa ni pamoja na vile vya korona kuenea.

Sisi na mazingira tunategemeana kabisa. Tusipoyatunza mazingira, hatuwezi tukajitunza.

Ni wakati wa Mazingira

Kutokana na uamuzi uliochukuliwa na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na Mkataba wa Bayoanuai ya Kibayolojia, UNEP na wabia wenza wanazindua Muongo wa Umoja wa Mataifa wa Kuboresha Mfumo wa Ekolojia (kuanzia mwaka wa 2021 hadi mwaka wa 2030). Huu ni mradi wa kimataifa wa kuboresha mahusiano kati ya binadamu na mazingira. UNEP pia inashirikiana na viongozi duniani kuanzisha mpango mpya wa Mfumo wa Kimataifa wa Bayoanuai Baada ya Mwaka wa 2020 ili kufikia Maono ya Mwaka wa 2050 ya Kuishi Vizuri na Mazingira.

Kuishi vizuri na mazingira kunawezekana tu iwapo tutaweza kukabiliana na athari ghasi zinazopelekea uharibifu wa bayoanuai na kutekeleza kikamilifu Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Mwaka wa 2030. Sherehe za kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani zitasaidia kuyafikia haya kwa kuleta pamoja jamii ya kimataifa na kuiwezesha kuchukua hatua zitakazoleta mabadiliko chanya.