Je, Siku ya Mazingira Duniani ni nini?

Siku ya Mazingira Duniani ni siku inayotambulika zaidi ya kushughulikia mazingira. Tangu mwaka wa 1974, imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka tarehe 5 mwezi wa Juni; ikileta pamoja serikali, mashirika ya biashara, watu maarufu na wananchi kushughulikia masuala nyeti ya mazingira.

Kauli mbiu

Katika mwaka wa 2020, kauli mbiu ni bayoanuai-suala linalopaswa kushughulikiwa kwa dharura. Matukio ya hivi karibuni, kuanzia kwa mioto ya misituni nchini Brazil, nchini Marekani na nchini Australia hadi kwa kuvamiwa na nzige katika maeneo ya Afrika Mashariki–na sasa, ugonjwa mtandavu wa kimataifa–vinaashiria kutegemeana kati ya wanadamu na viumbe wengine. Mazingira yanatupa ujumbe.

Jamii

La muhimu, Siku ya Mazingira Duniani ni jukwa la kimataifa la kuleta mabadiliko chanya. Hutambua kuwa mabadiliko ya kimataifa yanahitaji jamii ya kimataifa. Huhimiza watu binafsi kutafakari kuhusu kile wanachokila; kwa mashirika ya biashara kubuni mifumo isiyochafua mazingira; kwa wakulima na makampuni ya uzalishaji kuzalisha kwa njia endelevu; kwa serikali kuhifadhi makazi ya wanyamapori; kwa taasisi za elimu kuelimisha wanafunzi kuishi vizuri duniani; na kwa vijana kung'ang'ania hatima isiyochafua mazingira. Sote tunahitajika.

Mwenyeji

Kila Siku Ya Mazingira Duniani huadhimishwa katika nchi totauti ambayo hufanya maadhimisho rasmi. Mwenyeji wa mwaka huu ni nchi ya Kolombia.

Endelea Kutufuatilia

Mwaka huu, mamilioni ya watu watasherekea kupitia mtandaoni kote duniani. Jisajili hapa ili kujifahamisha zaidi tunapoungana kushughulikia mazingira.